Hebu tuzungumzie juu ya sheria. Paulo Mtumie aliwaambia Wayahudi walio ifuata sheria “kwa hiyo wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru, kwa maana katika hayo umhukumuye unafanya yale yale: Nasi twajua ya kuwa hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao hayo. Wewe binadamu uhukumuye je, wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu?” (Warumi 2:1-3). Waifuatao sheria hudhani kwamba wao ndio wanao mheshimu Mungu zaidi. Aina hii ya watu hawamwamini Mungu kwa mioyo yao yote, bali kwa majivuno yao bandia yaliyo katika msingi wa matendo yao. Watu hawa hupenda kuwahukumu wengine na ni wepesi kwa hilo sana. Hata hivyo wakiwa wana wahukumu wengine kwa maneno ya Mungu hawagundui ya kwamba wao nao wanafanana na hao wanao wahukumu na pia kufanya makosa hayo hayo.
https://www.bjnewlife.org/
https://youtube.com/@TheNewLifeMission
https://www.facebook.com/shin.john.35
Tunamwita Yohana, aliyembatiza Yesu, Yohana Mbatizaji. Sasa, nini maana ya ubatizo? “Ubatizo” kwa Kiyunani “babtizo” maana yake “kuzamisha” na maana kuu iliyo muhimu ya...
Akindelea kutoka sura ya 2, Mtume Paulo alitaja katika sura hii kwamba Wayahudi hawana upendeleo zaidi ya watu wa Mataifa. Katika sura hii, Paulo...
Je, wenye haki huishi kwa namna ipi? Kwa imani. Wenye haki huishi kwa imani. Ukweli ni kwamba neno “Imani” ni la kawaida, lakini ni...